www.themiyetu.blogspot.com. Powered by Blogger.

HABARI ZOTE

SIKILIZA REDIO HAPA

Translate

tangazo

tangazo

tangazo

tangazo

Mkapa yupo salama, kuibuka kesho kwa Magufuli

Wednesday, November 4, 2015

MSEMAJI Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa amefariki Dunia.

Akizungunza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwambene amesema Rais Mkapa yupo salama na mzima wa afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua.
 
Mwambene amewaasa watumiaji wa mitandao mbalimbali hasa Blogs kuacha kuitumia mitandao hiyo kwa kupotosha umma na kuandika nambo yasiyo na ukweli ili kuepusha mifumuko ya habari za upotishaji.
“Si jambo jema na wanaofanya hivyo waache mara moja kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa” amesema Mwambene.
 Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa
Amesema kuwa jambo la kumzushia mtu kifo si jambo zuri ambalo amelizungumza kama ‘uchuro’ kwa mtu husika na kumtabiria mabaya.
“Mkapa yupo hai na kesho pia atakuwepo katika sherehe za kumuapisha Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli,” amesema Mwmbene na kuongeza.
Serikali italishughulikia hili na tayari imeshaanza kukamata baadhi ya watu mbalimbali ambao wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma kupotoka.
Amesema kuwa vyombo vya habari vifanye kazi kwa uweredi ili kazi ya uandishi wao iwe ya usawa na kufuata misingi ya uandishi, jambo ambalo wengi hukiuka kutokana kutofuata weredi wa kazi zao.

Mazoezi ya kuapishwa Rais Mteule Dk. Magufuli yapamba moto Dar‏

Kibanda cha kitakachotumika wakati wa kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho kutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Maangu (wa tatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa wimbo wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 Maofisa mbalimbali  wakiwa katika kibanda cha kiapo wakipanga jinsi viongozi watakavyokaa wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wakati wa maandalizi hayo
 
Wasanii kutoka Zanzibar wakicheza ngoma ya kibati wakati wa mazoezi hayo.
 
Mtu aliyeigiza kama  Rais Jakaya Kikwete, akiwa amesimama alipokuwa akipigiwa mizinga ikiwa ni ishara ya kuagwa kwa rais huyo kabla ya kuapishwa Rais mpya wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli wakati wa mazoezi hayo.
 
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa Jukwaa Kuu wakati wa maandalizi hayo.
 
Baadhi ya wananchi na viongozi wa serikali wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa na Bendi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati wa maandalizi hayo.
 


Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akielekea kukagua gwaride la heshima la kumuaga wakati wa mazoezi hayo

Rais JK atangaza kesho kuwa sikukuu na siku ya mapumziko

rais-kikwete1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Ikulu newTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.
Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Novemba, 2015

DIWANI KATA YA THEMI MELANCE KINABO ASHINDA KWA ZAIDI YA 60%

Tuesday, October 27, 2015


Ni sikuchache baada ya uchaguzi mkuu, uliofanyika siku ya jumapili tarehe 25/ October 2015 ambapo wakazi wa Themi walikuwa na wajibu mkubwa sana wakuchagua kiongozi bora, mtendaji na mwenye kiu ya kufanya kazi.

 Kata ya Themi ilikuwa ikiwaniwa na wagombea watatu wa vyama vya CHADEMA, CCM na ACT wazalendo, ambapo Mhe. Melance Kinabo (Kaburu)  wa CHADEMA alitangazwa kuwa diwani mteule wa kata ya Themi baada ya kushinda kwa zaidi ya asilimia 60 dhidi ya wagombea wengine waliokuwa wakigombea kiti hicho cha udiwani.

Aidha Mhe. Diwani amewashukuru sana wananchi wa kata ya Themi kwa kumpa tena ridhaa ya kuwaongoza kwa mara nyingine, akizunguza na chombo chetu cha habari amesema "Nimekuwa diwani kwa muda mfupi sana, lakini utendaji kazi wangu umenipa fursa ya kukubalika na wananchi, na hii ninawaahidi kuwa nitawajibika kipindi hiki zaidi kuliko hapo awali" alisema.

mwananchi mmoja amabaye alijitambulisha kwa jina la ndg. Upendo kassariwa amesema kuwa "Mh. Kinabo hakuwa na mpinzania, isipokuwa kuwepo kwa vyama vingine ilikuwa ni sehemu tu ya vyama vingine kutaka tu kuwapa changamoto wananchi na kumjenga kisiasa Diwani wetu, maana walimtusi sana, walimkejeli lakini kutokana na kujitambua kwake na kutambua heshima yake kwa wananchi yeye aliwajibika kusema sera makini na kutangaza amani kipindi chote cha kampeni" alisema.

Mhe. Kinabo alimalizia kusema "Ninatambua matatizo ya kata yangu, natambua uhitaji wa wananchi wangu, kwa heshima kubwa nina waambia kuwa nitahakikisha ninatimiza ahadi zangu na kufanya yote kwa kumtanguliza kwanza Mungu. ninawaomba ushirikiano wao pale nitakapo uhitaji kwa maendeleo endelevu ya kata yetu, hususa katika maswala nyeti kama vile ulinzi wa mali zetu, miundo mbinu n.k"

HOJA YANGU: KWA UWAJIBIKAJI NA UADILIFU HUU WA MH. KINABO KUNAYO HAJA YA THEMI KUMPA RIDHAA YA KUONGOZA TENA

Friday, October 9, 2015

Mh. Melance E. Kinabo (anayetetea kiti chake cha udiwani)

 Themi ni miongoni mwa kata zeyenye rasilimali nyingi ikiwemo viwanda na uwanja wa maonesho ya siku ya wakulima (nane nane), Wakati Jiji la Arusha likitajwa kushikilia nafasi ya kwanza kwa  usafi kati ya Majiji yote Tanzania kwa mara ya kwanza, Themi nayo imekuwa miongoni mwa kata zilizo tajwa kuongoza kwa usafi 2013 - 2014 chini yauongozi wa Mh. Diwani Melance Kinabo, ikishikilia nafasi ya pili ndani ya halmashauri.
Robo tatu ya wakazi wa Themi sawa na 60% ni wafanyakazi wa viwandani na wengine waliobaki ni wafanyakazi katika maeneo mbalimbali. mwaka 2008 wafanyakazi wa kiwanda kilichokuwa kikizalisha matairi bora afrika mashariki walipewa taarifa ya kusimama kazi kwa madai kuwa kiwanda amepewa mwekezaji, jambo ambalo liliathiri wakazi wengi wa themi waliokuwa wakitegemea ujira huo kuendesha maisha yao.
Themi imebarikiwa kwa kuwa na viwanda vingi ikiwemo ABB, Kilitex, Sunflag, A to Z, Breweries, Genera tire n.k ambapo hivi sasa vingi vimeuwawa na serikali tawala baada ya kukabidhi wawekezaji na sasa kugeuka kuwa maskani ya vibaka na wacheza kamari, na kimojawapo kugeuzwa eneo la kanisa.
Ujio wa Mh. Melance Kinabo umekuwa ni faraja kubwa kwa Themi, amabapo aliongoza kwa kipindi cha miezi michache baada ya kuenguliwa kwa madiwani wanne wa chadema waliobainika kuwa walikuwa wakitumiwa na CCM baada ya kupokea rushwa kwa lengo la kumpitisha Meya wa Jiji la Arusha kutoka CCM.
Katikati ni Mh. Diwani wa kata ya Themi wakati akikabidhi Solar (umeme wa jua) katika kituo cha Afya Themi
 Mh. Kinabo katika kipindi kifupi cha uongozi wake amefanikiwa katika maeneo mbalimbali nayo ni;
Elimu
Mh. Kinabo amefanikiwa kuanzisha mpango maalum wa kusomesha watoto 2000 wanaotoka katikafamilia duni, kutoka shule za sekondari 10, na shule za msingi 10.
Na katika elimu yapo maeneo mawili ambayo ameyashughulikia, ambapo ni shule za msingi na sekondari.
Shule za msingi
Shule ya msingi Engira mh. Kinabo amefanikiwa kutekeleza robotatu ya ahadi zake zote ikiwemo,
Uchimbaji wa kisima cha maji na ufungaji wa pampu ya kupandisha maji, ambapo imepunguza adha kubwa ya upatikanaji wa maji kwaajili ya mazingira ya shule na mahitaji kwa wanafunzi.
Ujenzi na ukarabati wa madarasa mawili, ambapo yamejengwa kisasa zaidi na kugawanywa mawili kuwa ukumbi wa mikutano na lingine kuwa darasa maalumu la kompyuta.
Kurudisha umeme wa shule na kufanya baadhi ya shughuli zinazohitaji umeme kufanikiwa, kutokana na sehemu kubwa ya elimu na maisha ya sasa kutawaliwa na teknolojia.
Ukarabati wa choo cha matundu manne cha maji jambo ambalo limeifanya shule ya Engira kuonekana maridadi na haa kuwa vutia wanafunzi.
Aidha ufaulu wa wanafunzi wa Engira ulipanda kwa 100% 2013-2014, ambapo Mh. Diwani amekuwa akionesha ushirikiano katika kila hatua hususa kufadhili ziara za mafunzo mf. Ziara ya kutembelea hifadhi za wanyamapori ikiwemo Ngorongoro.
Shule ya msingi Themi pia Mh. Diwani amefanikiwa kutekeleza machache ikiwemo,
Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, na ununuzi wa mashine maalumu kwa ajili ya watu wasioona (Vipofu).
Ukarabati wa madarasa, na utengenezaji mashelfu kwaajili ya kuhifadhi vifaa vya masomo.
Ufaulu wa wanafunzi umeongezeka na kufikia 100% 2013-2014.
Shule za Sekondari
Shule ya sekondari Themi Mh. Diwani ametekeleza ahadi zake kwa zaidi ya asilimia 80%.
Ujenzi wa maabara tatu za kisasa
Upatikanaji wa eneo jipya la shule
Ukarabati na ununuzi wa vifaa vya shule ( ikiwemo madawati na viti)
Ujenzi wa geti na uzio wa shule
Ukamilishwaji wa ujenzi wa marasa manne ya ghorofa.
Kwa kiwango hicho mh. Diwani amechochea kusukuma maendeleo makubwa ya shule ya sekondari Themi, pia amekuwa akiwaombea wanafunzi misaada ya kiamasomo kupitia wadau mbalimbali, Taasisi za umma na Binafsi, ambapo ongezeko la ufaulu limekuwa kwa zaidi ya 65%
Shule ya Sekondari Arusha Day umefanyika ukarabati wa ofisi ya waalimu na maabara mbili, pamoja na ujenzi wa maabara nyingine ya kisasa, ujenzi wa uzio na geti la shule, pamoja na ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu kwa usalama wa wanafunzi na raia wengine.
Afya
Uwekwaji wa sola (umeme wa juwa) kituo cha afya imegharim, Pia kwa juhudi za Mh. Diwani umefanyika ukarabati wa vyoo na kuvifanya kuwa na miondombinu rafiki kwa wagonjwa. Uhamasishaji kwa kila familia kujiunga na afya ya jamii tiba kwa kadi (TIKA) inayogharimu Tsh. 12,000/= kwa mwaka. Aidha kwakutambua umuhim wa jamii na afya zao, Mh. Diwani amekuwa mstari wa mbele kutete huduma za afya kufanyika hadi siku ya jumamosi mpangoa ambao kwasasa umeridhiwa, Mh. Amehakikisha huduma ya mama na motto inakuwa salama na hivyo amekipatia kituo cha Afya Themi kitanda maalum na cha kisasa kwaajili ya kujifungulia akinamama wajawazito.
VIKUNDI
Vikundi vya akinamama kwa kuanzisha mradi wa akinamama Themi living garden, mradi huu unawasaidia akinamam wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, aidha umefanyika mchakato wa upatikanaji wa (12. M) kwaajili ya kuwakopesha vijana, na akinamama. Katika awamu ya Mh. Kinabo kumekuwa na ongezeko kubwa la uanzishwaji wa vikundi vya wajasiriamali katika Nyanja mbalimbali mfano vikundi vya sanaa, kuweka na kukopa n.k (kutoka vikundi 7, hadi kufikia 21).
MIUNDOMBINU
Umefanyika ukarabati wa ofisi ya Afisa mtendaji kata ya Themi na kurejeshwa umeme uliokuwa umekatwa kutokana na deni lililokuwepo hapo awali. Pia umefanyika ukarabati wa barabara za mitaa ya naenane, kambini, barabara ya Biya, kambarage, na ukarabati wa Barbara ya lami kutoka reline hadi uhasibu, kwa ushirikiano na kata ya Olorieni Mh. Amefanikiwa kujenga kivuko cha mtaa wa kambarage. Kufunguliwa na kutumika Barbara ya mount meru kupitia mahakama kuu, iliyokuwa imefunwa kwa muda mrefu.
HALMASHAURI
Ukuwaji wa mapato ya halmashauri kutoka 500 Million hadi 1.3 Billion.
Kufanya ushawishi wa serikali kununua mitambo maalumu kwaajili ya ujenzi wa miundombinu grader 1, compactor machine 1, na malori 3, kupatikana kwa hati safi baada ya miaka 5 ya hati zenye mashaka. ununuzi wa gari la wagonjwa (Ambulance), kushawishi na kutetea Arusha kuingizwa ktk (Master plan) mpango maalumu wa kuendeleza jiji la Arusha.
Haya ni miongoni mwa mafanikio ya Mh. Melance Kinabo katika kipindi chake cha uongozi, hivyo kwa kasi hii, uwezo na uthubutu aliouonesha ni dhahiri anakilasababu ya kupewa dhamana ya kurejea ili kuendelea kukamilisha mengine aliyoahidi na kukosa muda wa kutekeleza yote.
Themi inahitaji kurejesha heshima yake, kata hii inautajiri mwingi na iwapo serikali itakuwa makini katika kusimamia na kuweka mikakati yake vyema Themi inauwezo wakutengeneza zaidi ya 65% ya ajira kwa vijana wengi waliopo nchini wasio na ajira, pia inaweza kuwa kata pekee yenye kuchangia pato kubwa la Halmashauri kutokana na wingi wa viwanda vyake vilivyo uawa na wawekezaji.

Kwa kuzingatia sifa za uongozi bora Mh. Melance Kinabo ndiye  kiongozi mwana harakati na mtetezi wa Themi, kwakua anayoniya, uthubutu, sauti ya umma, msemaji na mtendaji mwaminifu.

MELANCE KINABO NI MFANISI NA MAKINI


Akiwa Diwani mteule wa kata ya Themi Jimbo la Arusha Mjini 2013 Ndugu Melance Kinabo (KABURU) kupitia CHADEMA, Kwa uchungu mkubwa alianza kazi zake rasmi kama diwani hili hali bado hakuwa ameapishwa.Leo tarehe 29 - June 2013 mishale ya saa tisa alasiri na kuwasili mtaa wa Fire maeneo ya magorofa ya polisi kusikiliza kilio cha akina mama ambao ni wakulima wa mbogamboga waliomuita kwa simu kumuomba msaada baada ya mwenyekiti wa Mtaa wa Themi Magharibi Mzee Dions Msele - CCM kukataza matumizi ya mfereji wa kumwagia maji ktk mashamba ya kina mama wa mtaa husika bila sababu za msingi.
 

Diwani huyu wa Themi kupitia Chadema  aliwahoji akina mama husika na kugundua kuwa Mwenyikiti wa mtaa hakuwa na sababu za msingi za kuwazuiya kina mama hao kuendelea na kilimo cha umwagiliaji kupitia mfereji husika.


Diwani huyu mteulealipofika kwa mtendaji wa kata ya Themi aligundua kuwa kina mama hawa wa Themi Magharibi wananyanyaswa na mwenyekiti wa mtaa Dions Msele - CCM na ndipo akatoa amri kuwa mfereji huo ufunguliwe na kina mama waendelee na kilimo cha mboga bila kusumbuliwa na kutoa ahadi ya kusimamia utengenezaji wa kalavat kwenye mfereji husika kuepusha ajali kwa watoto wa polisi wanaoishi maeneo ya Themi Magharibi karibu na chanzo cha mfereji huo ulioleta utata jambo ambalo limekwisha shughulikiwa.

Aidha mwanachi mmoja amabaye hakutaka jina lake litajwe wakati akihojiana na mwandishi wetu alisema kuwa wananchi wa Arusha wanajua Rais ni Lowassa, Mbunge ni Lema na Diwani wa Themi ni Melance Kinabo, hakuna asiyejua ufanisi na umakini wake wa utendaji, niseme tu viongozi hawa ni wawajibikaji, wazalendo na watu makini.
  
 
Hivi ni moja ya vipaumbele vya Mh. Kinabo katika ahadi zake iwapo wananchi watampa ridhaa tena ya kuwaongoza na kuwa Diwani wa kata ya Themi mwaka 2015-2020.
  • AFYA
Kujenga uzio na kukamilisha maboresho yote ya kituo cha Afya Themi, ikiwemo ujenzi na ufungaji mashine ya kuchoma taka za Hospitali, ujenzi wa chumba cha upasuaji kina mama wajawazito, na ununuzi wa Gari la wagonjwa (Ambulance).
  • MIUNDOMBINU NA MIPANGO MIJI
 Upatikanaji wa maeneo ya wazi kwajili ya biashara za vijana na akinamama. Kupata upimaji wa maeneo mbalimbali ndani ya kata ( Mtaa wa Kambarage), ukarabati na ujenzi wa barabara zote za kata, ikiwemo Serengeti (mtaa Corridor area, pamojana Engira road, na Barabara za AICC Flats), kufungua barabara zinazounganisha kati ya mtaa kwa mtaa na kata kwa kata. kuongeza nguvu za kisheria katika kuimarisha na kuboresha miundombinu ya AICC barabara na nyumba, pia upatikanaji wa maji safi  na salama kwa uhakika, mfano mtaa wa AICC, Themi mashariki na Kambarage. Aidha kujenga, na kutetea kwa nguvu zote hoja  ya ukarabati wa nyumba za polisi (Old polisi fire) chombo ambacho ni muhimu sana kwa raia na mali zao. 
  • ELIMU
Jinsi ya kumsaidia Mtanzania ni kumpa Elimu.  Alisema Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh. Cristopher Kongoye alipokuwa akimshukuru Mh. Diwani wa Themi Melance Edmund Kinabo na kuungana nae kwa kusema, tunawaitaji watu wanaoleta maendelea kama wewe na kumwaidi kumpa ushirikiano wa kutosha na kusema hataitaji watu mizigo kwenye maendeleo.
Kwakutambua hilo, Mh. Kinabo ameongeza msimamo wake na kuahidi kusimamia upatikanajii wa shule ya ufundi kwaajili ya vijana katika shule ya msingi Engira.
Ufuatiliaji na usimamizi thabiti ili kupatikana kwa eneo la ujenzi wa shule ya msingi kati ya kata ya Engutoto na Mtaa wa kambarage.
Ujenzi wa ukuta wa shule ya msingi Engira pamoja na kukamilisha ujenzi na ukarabati wa Shule ya sekondari Themi na shule ya msingi Themi.
Kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanakwenda shule.

 
  • UCHUMI
Kuwezesha vikundi vya  VICOBA kuwa SACCOSS
Kuanzisha/ kuunda kongamano la mafunzo kwaajili ya vijana (Ujasiriamali)
Kutambua makundi maalum na kuweza kuwasaidia
Kuunda timu ya soka kata ya Themi.
  • ULINZI NA USALAMA
 Kuhakikisha kuwa vinaundwa vikundi vya vijana kwaajili ya ulinzi shirikishi, ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao ndani ya kata ya Themi.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. THEMI YETU - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Inspired by Sportapolis Shape5.com
Proudly powered by Blogger